Sawa.
[Caveat: The following is some detailed advice about contributing to the
Swahili wikipedia, esp. how to avoid Google translator due to problems of
over-writing articles and how to use some wiki conventions.]
Nina jambo lingine kuhusu J'mosi ya Wikipedia. Mkichangia makala za
Kiswahili ( <http://sw.wikipedia.org/>
http://sw.wikipedia.org) msitumie
kitambo cha utafsiri cha Google (
http://translate.google.com/toolkit/)
ovyoovyo. Kwanza lazima kuhakikisha kwamba makala lengwa haijaandikwa bado.
Msipofanya hivyo mngeweza kufuta habari ambazo zimeshaingizwa na mwingine.
Ndivyo ilivyofanyika k.m. jana tu na makala ya mwandishi wa Kenya Marjorie
Oludhe Macgoye, angalieni hapa:
http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Marjorie_Oludhe_Macgoye
<http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Marjorie_Oludhe_Macgoye&diff=next
&oldid=545629> &diff=next&oldid=545629
Ni kweli, kwa sehemu mtafsiri wa Google wa jana aliboresha makala ya tarehe
16 Novemba 2010 ila kwa sehemu kubwa zaidi aliiathiri vibaya, k.m. [[Jamii]]
zote zilirudishwa kwenye [[Category]], tena "category" za uongo; pia kiungo
cha [[fi:]] kilifutwa na mambo mengi mengineyo. Msifanye hivyo. Ni matumizi
ya ovyo kama hayo ambayo yamemkasirisha mzee wetu wa wikipedia Kipala. Naye
ni "bureaucrat" kwa hivyo mtamtegemea mara kwa mara kuwasaidieni.
Msimkasirishe. Asanteni!
Kwa mashauri mengine, angalieni nilivyomwandikia ndugu yetu Limoke mwaka
jana (
http://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_mtumiaji:Mpmayenge):
Ndugu Limoke, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila
kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya
kurekebisha sana. Kwa hiyo sasa, naomba tusaidiane kusawazisha hizo makala.
Kwa mfano, ungeweza kuanza kwa kuangalia orodha ya makala
<http://sw.wikipedia.org/wiki/Maalum:KurasaZisizonajamii> bila jamii. Bila
shaka utagundua kadhaa ambazo ni duni, labda yenye maneno mawili matatu tu.
Ndivyo nilivyogundua k.m. na makala ya Henri Fayol
<http://sw.wikipedia.org/wiki/Henri_Fayol> , mhandisi Mfaransa wa karne ya
19. Sasa ukiangalia mabadiliko
<http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Henri_Fayol&action=historysubmit&
diff=364028&oldid=337882> niliyoyaingiza utapata mambo ya msingi ya
wikipedia. K.m. naingiza kigezo cha {{DEFAULTSORT}} kwa ajili ya orodha ya
makala katika jamii ifuate alfabeti vizuri. Tena naingiza jamii za miaka ya
kuzaliwa (k.m. [[Jamii:Waliozaliwa 1841]]) na ya kufariki (k.m.
[[Jamii:Waliofariki 1925]]). Pia, ikiwa ni makala fupi bila maelezo mengi,
naingiza kigezo cha {{mbegu-mtu}} (yaani kama ni mtu). Hatimaye, naingiza
kiungo kwa wikipedia ya Kiingereza (k.m. [[en:Henri Fayol]]) ambapo naweza
kupata code kwa picha ya mtu (k.m. [[Image:Fonds henri
fayol.jpg|thumb|right|Henri Fayol]]) pamoja na habari nyingine. Nitashukuru
kwa msaada wako katika kuboresha makala mpya zilizoachwa duni. Wasalaam,
--Baba Tabita <http://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Baba_Tabita>
(majadiliano
<http://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_mtumiaji:Baba_Tabita> ) 07:17,
3 Februari 2010 (UTC)
Ndugu Limoke, asante kwa jibu lako. Nimefurahi kusikia kuwa utaendelea.
Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia baada ya
shindano. Sababu hasa ni kwamba tukiendelea kuboresha makala zilizoongezeka,
tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala fulani,
lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia
k.m. makala ya <http://sw.wikipedia.org/wiki/Uchumi> uchumi. Ukiihariri
bila kuangalia <http://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano:Uchumi>
majadiliano yake wala
<http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Uchumi&action=history> historia
yake, inawezekana utaongeza kazi ya baadaye kwa vile tafsiri za shindano
zilizofuta makala za zamani (pamoja na jamii na interwiki zake)
hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama hiyo na kuziandikia
katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri mbili au zaidi,
labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake, na
kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na
kazi. Na asante kwa kazi yako. (Pia, ukiandika kwenye kurasa za majadiliano,
ungeweza kutia sahihi kwa kutaipu ~~~~ ukiwa umesajiliwa kama
<http://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Limoke_oscar> Limoke oscar.)
Wasalaam, -- <http://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Baba_Tabita> Baba Tabita
( <http://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_mtumiaji:Baba_Tabita>
majadiliano) 04:08, 4 Februari 2010 (UTC)
Mkiangalia historia ya makala ya uchumi iliyotajwa hapo juu, mtaona kwamba
tafsiri zote za "Challenge" zilirejeshwa. Tusifanye kazi bure walivyofanya
hao.
Sina lingine kwa sasa ila kuwatakieni mafanikio mema siku ya J'mosi ya
Wikipedia. Asanteni!
Ni mimi, Baba Tabita (aka Oliver)
_____
From: Abbas Mahmood [mailto:abbasjnr@hotmail.com]
Sent: 21 April 2011 19:28
To: oliver_stegen(a)sil.org; 'The discussion list for the upcoming Wikimedia
Kenya chapter.'
Subject: RE: [Wikimedia Kenya] WikiSaturday
It is supposed to be on 30th.
_____
From: oliver_stegen(a)sil.org
To: wikimediake(a)lists.wikimedia.org
Date: Thu, 21 Apr 2011 19:06:56 +0300
Subject: Re: [Wikimedia Kenya] WikiSaturday
I understood WikiSaturday to be on April 30, not April 23 . ?!?
Alex, for when have you booked iHub?
In any case, I may have to join you from home as family usually keeps me
occupied on Saturdays.
Oliver (aka BT)
_____
From: wikimediake-bounces(a)lists.wikimedia.org
[mailto:wikimediake-bounces@lists.wikimedia.org] On Behalf Of SAMSON MAOSA
Sent: 21 April 2011 17:01
To: The discussion list for the upcoming Wikimedia Kenya chapter.
Subject: Re: [Wikimedia Kenya] Survey
Greetings all, hoping everyone is contented now. Speaking of WikiSaturday,
since I am far from Nairobi I will start mine tomorrow. Whether it is
Tomorrow I will do Swahili Wikipedia and on Saturday, if I get internet,
will do English Wikipedia. Have a good friday all.
--
____________________________________________________________________________
______
Samson Arosi Maosa,
Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology,
Bsc. Electronics and Computer Engineering
+254750-nine-one-seven-three-zero-five
"In this world, everything has been done but suppose we try doing it in a
different (better) way?"
Make someone know what you already know. Join us now at Wikimedia Kenya
<http://www.wikimedia.or.ke>
_______________________________________________ WikimediaKE mailing list
WikimediaKE(a)lists.wikimedia.org
https://lists.wikimedia.org/mailman/listinfo/wikimediake