Sawa.
[Caveat:
The following is some detailed advice about contributing to the Swahili
wikipedia, esp. how to avoid Google translator due to problems of over-writing articles
and how to use some wiki conventions.]
Nina jambo lingine kuhusu J’mosi ya
Wikipedia. Mkichangia makala za Kiswahili (http://sw.wikipedia.org) msitumie
kitambo cha utafsiri cha Google (http://translate.google.com/toolkit/)
ovyoovyo.
Ni kweli, kwa sehemu mtafsiri wa Google wa
jana aliboresha makala ya tarehe 16 Novemba 2010 ila kwa sehemu kubwa zaidi aliiathiri
vibaya, k.m. [[Jamii]] zote zilirudishwa kwenye [[Category]], tena “category”
za uongo; pia kiungo cha [[fi:]] kilifutwa na mambo mengi mengineyo. Msifanye hivyo. Ni matumizi ya ovyo
Kwa mashauri mengine, angalieni
nilivyomwandikia ndugu yetu Limoke mwaka jana (http://sw.wikipedia.org/wiki/Majadiliano_ya_mtumiaji:Mpmayenge):
Ndugu Limoke, salaam! Wakati wa shindano, makala nyingi zimeanzishwa bila
kuwekewa yaliyomo hata kidogo, nasi wanawikipedia hatukuwa na nafasi ya
kurekebisha
Ndugu Limoke, asante kwa jibu lako. Nimefurahi kusikia
kuwa utaendelea. Unisamehe nikiendelea kuandika kuhusu usafishaji wa wikipedia
baada ya shindano. Sababu hasa ni kwamba tukiendelea kuboresha makala
zilizoongezeka, tuwe makini. Kabla hatujaongeza au kurekebisha habari za makala
fulani, lazima tuangalie majadiliano na ukurasa wa historia ya makala hiyo. Angalia
k.m. makala ya uchumi. Ukiihariri bila kuangalia majadiliano yake wala historia yake, inawezekana utaongeza kazi ya
baadaye kwa vile tafsiri za shindano zilizofuta makala za zamani (pamoja na
jamii na interwiki zake) hazijaunganishwa. Nitaendelea kutafuta makala kama
hiyo na kuziandikia katika majadiliano yake. Kwa ajili ya kuunganisha tafsiri
mbili au zaidi, labda itasaidia ukifungua zote, kila moja katika dirisha lake,
na kunakilisha sehemu za makala za zamani kwenda katika makala ya sasa. Pole na
kazi. Na asante kwa kazi yako. (Pia, ukiandika kwenye kurasa za majadiliano,
ungeweza kutia sahihi kwa kutaipu ~~~~
ukiwa umesajiliwa kama Limoke oscar.) Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 04:08, 4 Februari
2010 (UTC)
Mkiangalia historia ya
makala ya uchumi iliyotajwa hapo juu, mtaona kwamba tafsiri zote za „Challenge“
zilirejeshwa. Tusifanye kazi bure walivyofanya hao.
Sina lingine kwa sasa ila
kuwatakieni mafanikio mema siku ya J’mosi ya Wikipedia. Asanteni!
Ni mimi, Baba Tabita (aka
Oliver)
From:
Abbas Mahmood [mailto:abbasjnr@hotmail.com]
Sent: 21 April 2011 19:28
To: oliver_stegen@sil.org; 'The
discussion list for the upcoming Wikimedia
Subject: RE: [Wikimedia
It is supposed to be on 30th.
From: oliver_stegen@sil.org
To: wikimediake@lists.wikimedia.org
Date: Thu, 21 Apr 2011 19:06:56 +0300
Subject: Re: [Wikimedia
I understood WikiSaturday to be on April
30, not April 23 … ?!?
Alex, for when have you booked iHub?
In any case, I may have to join you from
home as family usually keeps me occupied on Saturdays.
Oliver (aka BT)
From:
wikimediake-bounces@lists.wikimedia.org [mailto:wikimediake-bounces@lists.wikimedia.org]
On Behalf Of SAMSON MAOSA
Sent: 21 April 2011 17:01
To: The discussion list for the
upcoming Wikimedia Kenya chapter.
Subject: Re: [Wikimedia
Greetings all, hoping
everyone is contented now. Speaking of WikiSaturday, since I am far from
--
__________________________________________________________________________________
Samson Arosi Maosa,
Bsc. Electronics and Computer Engineering
+254750-nine-one-seven-three-zero-five
"In this world, everything has been
done but suppose we try doing it in a different (better) way?"
Make someone know what you
already know. Join us now at Wikimedia Kenya
_______________________________________________ WikimediaKE mailing list
WikimediaKE@lists.wikimedia.org
https://lists.wikimedia.org/mailman/listinfo/wikimediake