Date: Sun, 26 Jun 2011 16:03:57 +0300
From: oslimoke(a)gmail.com
To: wikimediake(a)lists.wikimedia.org
Subject: [Wikimedia Kenya] Mwito wa Maelewano
Kwa Wapenzi na Wapambe wa WMKE
Wasaalam kutoka kwangu nikitarajia mpo vyema.Dhamira yangu ya kuandika
barua hii ni kuwasii enyi wapenzi na wapambe wa WMKE tuwe na maelewano
na kushirikiana katika shughuli zetu a kuendeleza ukuajia wa Wikipedia
na usambazaji wa habari kwa wote
==Mizozo==
Mara si haba nimetazama tukizomeana vikali(miye nkiwemo) katika nyuzi
kadhaa a barua pepe.Swali langu ni kwa nini tuzomene ilhali sote
tumejitolee kwa hiari kuandeleza usambai wa habari?pengine wengine
wetu hatufahamu ni kwa nini tupo kwenye kundi hili le WMKE...hilo ndo
jibu nimeng'amua kwa uchungu.kwa nini?ukitazama kwa umakini,nyuzi
ziletazo udhia na tafash ni zile zilizo za kitu fulani,yaani
"faida".utapata kila watu wachangia katika uzi huo sana.kinachokera
sana ni tunapokuwa na uzi wa kung'amua na kuchangunua makala au miradi
inayoohusu WMKE(kama vile Bylwas,WTN) nk,ni wachache sana hujitokea
kuchangia kwa miradi hizi.Ilhali miradi hii haswa ndio maana ya kuwepo
kwa WMKE na sio zile a "faida"
==kukosoana==
Ni vyema kukosoana kila mara tunapoteleza.Miye nafurahi kukosolewa au
mtu kukosoa mawazo au michango yangu.Lakini nadhani ingekuwa vyema
tukosoane kwa heshima na pia toa suluhu au wazo mbadala,sio tu
kunikosoa bila sababu.
==Heko==
Mara nyingi tumesaha jinsi ya kuwapa na kutia watu motisha.Ningepende
tusikosoane tu,bali kuwapongeza wenzetu na kuwapa heko kwa kazi nuri
walo/wafanyazo.Hekow huwatia watu motisha wa kuendela kufanya
vyema.Kwa hayo,miye binafsi ningependa kuwatia wafuata heko kwa kazi
yao/michango yao katika kukua miradi na WMKE
*Abbas-anashughulika maswala ya sheria(Bylaws) na pia anauunda
wavuti(website) wetu kwa sasa...heko Abbas:-)
*Alex-anashughulika mawsala ya WTN na pia yeye alitutengezea posta
maridadi ya WikiSaturday ya JKUAT...kazi nzuri Alex
*Steve-alisughulika na kuanda makala ya WikiSaturday ya JKUAT na pia
ni mshrika mkuu.Alipiga chapa na kusambaza posta za WikiSaturday kwa
kutumia hela ake...Heko Steve
...kama sijakutaja samahani,sijataka kuwahudhi watu na barua
refu...sku nyingine na sijakusudia.
Tafadhali:Nawaomba wanachama kutazama wavuti wa Wikipedia Takes
Nairobi
Hapa:http://en.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Wikipedia_takes_Nairobi/Goals
na kuchangia ili tufanikishe mradi huu.
Pia naomba wanachama watazame makala ya Abbas ya Sheria na kuyapiga
msasa na kuchanganua kabla yatumwe kwani hizi ndizo sheria zitakazo
tuongoa na ni vyuema kutoa mchango wako.
Mwsiho tazama wavuti wetu hapa:
http://wikimedia.or.ke/Visit_of_Asaf_Bartov_from_the_Wikimedia_Foundation
ili tujadiliane kuhusu kuja kwa Asaf na vile twaweza kufaidi kwa ziara yake.
p/s:nimetumia Swahili maana haya ni mambo yetu ya "ndani",..-)
--
Limoke Oscar,
_______________________________________________
WikimediaKE mailing list
WikimediaKE(a)lists.wikimedia.org
https://lists.wikimedia.org/mailman/listinfo/wikimediake