Hamjambo,
Kwa miezi michache iliyopita, tumekuwa na ugumu wa majadiliano/mawasiliano kati yetu na washirika wenye malengo sawa na yetu kama vile google, ICT board.
Tumekuwa tukiwatumia barua pepe ili tushirikiane katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ilhali wanatuchukua kana kwamba tuna mchezo.
Sijui ni kwa sababu sisi ni wanafunzi, vijana ama kwa sababu zingine ambazo wao wenyewe wanazilelewa vyema zaidi.
* Ningeonelea kwamba, panapo wezekana tufanye miradi yetu bila ya hata kuwajulisha ila tu waone ama waskie miradi hii katika magazeti na kusikiza maredio..
* Kuwahusisha imedhihirisha kwamba wamekuwa mizigo badala ya usaidizi kama tulivyo taraji.
* Mbona Google wanarudisha majibu ya barua pepe mara tu mwakilishi wa wakfa wa Wikimedia anapowatumia barua pepe kama vile Asaf?? Ilhali hawafanyi hivyo wakati mwanachama wa WMKE anapojaribu kuwasiliana nao.
Kutoka sasa naonelea tufanye miradi yetu kivyetu na bila shaka tutafaulu kama tulivyo fanya katika kumbukumbu ya Wikipedia 10 na mradi wa Wikipedia for Schools
Kwa hayo mafupi naonelea tufungue anwani za barua pepe zinazoishia na wikimedia.or.ke tujaribu kuona vile washirika hawa watatuchukulia.
Mimi wenu, Wathika Wanjau
iwanjau.blogpost.com @uwanja www.facebook.com/swanjau